Juacali (Baba Yao) ft. Juliani - Si Siri (OFFICIAL VIDEO)

  • Juacali (Baba Yao) ft. Juliani - Si Siri
    Beat ya Clemo
    Dir: Charles Luche / Calif Pictures
    SI SIRI LYRICS
    Verse 1: Jua Cali:
    Mungu mi nashuru pahali umetufikisha
    na blessings zote umetupatia
    kufika miaka thirty si mchezo
    kufika hapa mahali tumefika si mchezo
    nakumbuka tukifoot mpaka mguu inauma
    tukikula skuma mpaka tumbo inafura
    ama tukikaa ubao sababu ngoma imetushika
    hio ni sauti yangu kwa CD hebu rudia
    hatuna machine tunalipia studio time
    Clemo tukona 2HRS ya kurecord wacha ni rhyme
    hizi vocals zinasound safi
    time kwisha tunamix hii ngoma mtaani
    Mungu ametubless tukona keyboard yetu saa hii
    Ametubless tukona studio yetu saa hii
    Ametubless tunajisimamia saa hii
    na Ametubless zaidi na maskio ya watu mtaani
    we si unajua venye kufurahisha watu ni ngumu
    kwa hivyo kabla tutoe hii ngoma nashukuru Mungu
    na familia zetu kutupatia nguvu
    na kusimama nyuma yetu kwa hii industry sumu
    tunahustle jamaa chuki ya nini
    tunajaribu jamaa mangumi ni za nini
    mapromoter wengine ndio wako na njaa
    kwanza wa Busia wanavuka boarder ka Jaguar
    haina noma mi hukumbuka mvumilivu
    akijiamini sana ye hula mbivu
    ona saa hii ma corporate wakona sisi
    ma account zinanyemelea amilli
    CHORUS LYRICS:
    Maisha inatubamba si siri
    eeh
    si siri
    maisha inatubamba si siri
    si siri, si ringi...
    VERSE 1 LYRICS:
    Juliani:
    Chuo tulipata D-, kwa life tulikuwa less
    God Akatupa B ikawa Blessing
    jeans buggy marvin
    walidhani kwa kichwa mavi in
    tuko rate ya 4.6
    shati imelaliwa na crusifix
    shati imelalia God within
    hatujavunja law isipokuwa ya gravity
    tunafly nikaa tuliokota feather moja kwa wing
    ya angel Gabriel
    price tag ya mimi, Bill Gates anabargain
    inatake msalaba, damu stain
    ipasuke mara mbili curtain
    sasa sisi saa vipi surplus uwingi
    cheki kipara akiingia kinyozi
    ni ka nywele inamea kwa kichwa pekee
    warembo wanabreath hewa nyingi
    wana extra rib
    si excuse niki fail
    nakam through times two nitahave ku
    na siachi, ka Agagbo wa Ivory Coast
    CHORUS LYRICS:
    Si siri, si ringi...
    Maisha inatubamba si siri
    eeh
    si siri
    maisha inatubamba si siri
    si siri, si ringi...

    Category : Kenya Music Videos

    #juacali#baba#yao#ft#juliani#si#siri#official#video

    0 Comments and 0 replies
arrow_drop_up