MZALENDO- NASOGEA GOLIGOTA

 • Sio kweli kua sina watoto, mke wala wazazi ambao napaswa kujiuliza ntawaachaje nikiondoka wapo na najua watapata taabu zaidi lkn kwa ajili ya Tanzania yangu sinabudi kujitoa kwa lolote lile liwalo na liwe.
  Nikifa kwa ajali au ugonjwa kitakua kilio na huzuni kwa ndugu na rafiki zangu lakini nikifa kwa kuitetea Tanzania kitakua kilio cha taifa zima la wapenda haki na amani alioiacha baba wa taifa letu Nyerere.
  Kama tuaminivyo Wakristo bwana wetu Yesu Kristo alisogea Goligota siku kama ya leo kwa ajili ya kutuokoa sisi tupate kusamehewa dhambi zetu, basi nami pia nachukua fursa hii kusogea nae GOLIGOTA kwa ajili ya kuitetea Tanzania na kukemea maovu yote yanayoendelea ktk serikali hii ya awamu ya 5
  MUNGU KAA NAMI MPAKA MWISHO

  Category : Tanzania Music Videos

  #mzalendo#nasogea#goligota

  0 Comments and 0 replies
arrow_drop_up